Thursday, June 21, 2012

Uwajibikaji wa Wanyama

<><>
Kila kukicha,

Swala huamuka.

Hutambua kuwa ni lazima akimbie kwa kasi kuliko Simba akimbiaye kwa kasi zaidi la sivyo atauwawa.

Kila kukicha,

Simba naye huamuka.

Hutambua kuwa ni lazima amkimbize Swala mwenye kasi ndogo kuliko wote la sivyo atakufa njaa.

Haijalishi wewe ni Swala au Simba.

Jua linapochomoza,

Ni bora uanze kukimbia kabla hujakimbizwa.

No comments:

Post a Comment