Hii picha ilichukuliwa wakati ujenzi ukiwa kwenye hatua za mwisho Oktoba, 2011.
Hiki ni Chuo kilichopo Kyela Mjini kinachotarajiwa kuanza mafunzo kwa fani mbalimbali kuanzia mwezi Agosti, 2012. Hivyo kila mdau anakaribiswa kutafuta fomu za kujiunga kabla nafasi hazijaisha.
Chuo hiki kitakuwa moja kati ya vyuo bora kabisa kanda ya Kusini na Nchi jirani, natoa rai kwa wazazi kuwapeleka vijana wao kuanza masomo kwani ukichelewa utakuta vijana wa Nchi ya jirani (Malawi) wamejaza nafasi.
Nawapongeza The Mango Tree kwa juhudi zao za kuanzisha Chuo hiki. Hii itakuwa fursa kwa wadau wengine kuwekeza katika Wilaya ya Kyela hasa kwenye sekta ya elimu, ikizingatiwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa chuo cha Ualimu katika Wilaya hii.
Kwa taarifa zaidi tembelea www.themangotree.org/Tanzania
Tanzania kuna vivutio vingi sana, cha msingi ni kuviendeleza na kuvitangaza zaidi.
ReplyDelete